HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 5, 2016

BALOZI WA TANZANIA NCHINI KENYA ASHIRIKI KUJADILI JINSI YA UDHIBITI WA MADAWA YA KULEVYA.


Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule (Kushoto), akizungumza na Mkurugenzi wa Mashariki mwa Afrika wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Uhalifu, Bw. Jose Vila De-Castillo, alipotembelea Ubalozini, jijini Nairobi, jana. Bw. De-Castillo aliomba Ubalozi uwe kiungo kati ya Taasisi yake na Serikali ya Tanzania. 

Taasisi hiyo inaendesha mpango wa miaka mitano wa udhibiti wa rushwa, mitandao ya uhalifu, biashara na matumizi ya madawa ya kulevya, ujangili na biashara ya binadamu kwa nchi za Tanzania, Burundi,Comoro, 
Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Madagascar, Mauritius, Rwanda, Seychelles na Somalia. Kulia ni Ofisa wa Ubalozi, Bw. Mussa Haji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad