HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 30, 2015

SHULE YA MSINGI MLIMANI YAUNGANISHWA NA MTANDAO WA INTANETI

Baadhi ya wanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Mlimani iliyopo Wilayani jijini Dar es Salaam wakijifunza somo la kompyuta baada ya kuunganishwa na mtandano wa Intaneti bure kwa msaada wa Vodacom Foundation wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika shuleni hapo leo na kuzinduliwa na Ofisa Mkuu wa Mtandao wa kampuni hiyo,Alec Mulonga(hayupo pichani).Vodacom imeanzisha mkakati wa kuleta mabadiliko kwa jamii ya Tanzania katika kupitia Teknolojia.

Ofisa Mkuu wa Mtandao wa Vodacom Tanzania,Alec Mulonga(kulia)akibofya kitufe cha kompyuta ikiwa ni ishara ya kizindua mtandao wa Intanet uliounganishwa katika Shule ya Msingi Mlimani ya jijini Dar es Salaam kwa msaada wa Vodacom Foundation,kwa ajili ya wanafunzi kujifunza somo la Kompyuta na kunufaika na masomo mbalimbali kupitia kuperuzi intaneti.Anayeshuhudia kushoto ni Kaimu Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Rosalynn Mworia. Vodacom imeanzisha mkakati wa kuleta mabadiliko kwa jamii ya Tanzania katika kupitia Teknolojia.

Ofisa Mkuu wa Mtandao wa Vodacom Tanzania, Alec Mulonga (kulia) akiwafafanulia jambo wanafunzi wa darasa la tano wa shule ya msingi Mlimani jijini Dar es Salaam,wakati wa uzinduzi wa mtandao wa Intaneti uliounganishwa na kampuni hiyo bure shuleni hapo,kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo kujifunza somo la Kompyuta na kunufaika na masomo mbalimbali kupitia kompyuta hizo.Anayeshuhudia kushoto ni Kaimu Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Rosalynn Mworia. Vodacom imeanzisha mkakati wa kuleta mabadiliko kwa jamii ya Tanzania katika kupitia Teknolojia.


Mhandisi Mwandamizi wa Mtandao wa Vodacom Tanzania,Frank Kasati akiwaonyesha wanafunzi wa shule ya msingi Mlimani kifaa maalum kinachoosambaza mtandao wa intaneti shuleni hapo wakati wa uzinduzi wa mtandao wa Intaneti uliounganishwa na kampuni hiyo bure shuleni hapo kwa msaada wa Vodacom Foundation,kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo kujifunza somo la Kompyuta na kunufaika na masomo mbalimbali kupitia mtandao huo. Vodacom imeanzisha mkakati wa kuleta mabadiliko kwa jamii ya Tanzania katika kupitia Teknolojia.


WANAFUNZI  wa Shule ya Msingi ya Mlimani iliyopo eneo la Chuo Kikuu cha jijini Dar es Salaam wameonekana kuwa na furaha wakati wakiperuzi mtandao wa intanet kwenye kompyuta zao zilizopo kwenye chumba cha kujifunzia somo hilo shuleni hapo wakati wa hafla ya uzinduzi wa matumizi ya intanet katika kujifunza uliofanyika leo shuleni hapo.Msaada wa kuunganishwa na mtandao wa intaneti umetolewa na taasisi ya Vodacom Foundation baada ya kutoa msaada wa kompyuta hizo miezi mitatu iliyopita. Vodacom imeanzisha mkakati wa kuleta mabadiliko kwa jamii kupitia Teknolojia. 

Wanafunzi wa Mlimani wameungana na wenzao wapatao 5000 kutoka shule nyingine za msingi na sekondari nchini ambao wanapata elimu ya matumizi ya kompyuta kwa vitendo na kuweza kujifunza masomo mbalimbali kwa njia ya mtandao. 

Vodacom Foundation kwa kushirikiana na taasisi isiyo kuwa ya kiserikali ya Learning In Sync zilizindua mradi huu mwaka 2013 unaojulikana kama”Smart school program”na tayari umeanza kuleta mafanikio makubwa kwa kuwawezesha baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari jijini Dar es Salaam kuingia katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.Shule ambazo zimenufaika na mradi huu ni Makumbusho,Kinyerezi,Mtakuja na Kambangwa na shule ya sekondari Shimbwe iliyopo Uru Moshi vijijini. 

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mlimani Pendo Kujelwa ameshukuru kwa msaada huu na kusema kuwa mradi huu ni muhimu na utawawezesha wanafunzi katika shule yake kuingia katika ulimwengu wa kompyuta na hivi sasa wanaweza kumudu vizuri somo hilo kwa kuwa wanalisoma kwa nadharia na vitendo na kupata maarifa mbalimbali kupitia mtandao wa intanet. 

Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake Martha Mtweve anayesoma darasa la sita shuleni hapo alishukuru kwa msaada na kusema utawasaidia kujua somo la kompyuta na kupata maarifa kupitia intanet na alishukuru taasisi ya Vodacom Foundation kwa ufadhili huu. 

Akiongea wakati wa hafla hiyo,Mkuu wa Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza alisema “ Siku zote tutakuwa mstari wa mbele kuhakikisha vijana wa kitanzania wananufaika na mtandao wetu kwa kuwapatia elimu bora kupitia mawasiliano na teknolojia ya kisasa.Mpango huu unawawezesha vijana kupata elimu bora na kuwaunganisha na wenzao sehemu mbalimbali duniani kote ambapo wanaweza kupata taarifa mbalimbali na maarifa kwa urahisi. 

Alisema Vodacom inafanya kila jitihada kuhakikisha inaendeleza jamii katika nyanja mbalimbali kupitia mawasiliano na teknolojia hususani kwa vijana ambao wanapaswa kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ambayo ndiyo yanatawala katika ulimwengu wa sasa wa Sayansi na Teknolojia. 

“Mawasiliano mazuri huwezesha watu kupata taarifa mbalimbali zinazotokea katika mazingira yao walipo na sehemu za mbali kwa urahisi.Kwa wanafunzi kompyuta zinasaidia sana kupata maarifa kupitia mtandao wa internet.Nawahasa wanafunzi wa Mlimani msome kwa bidii na mtumie vizuri fursa hii kutafuta elimu na msiogope kusoma masomo ya sayansi maana mambo yote hivi sasa yamerahisishwa kupitia teknolojia hii ya kompyuta”.Alisema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad