HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 24, 2015

WANANCHI VIJIJINI KUNUFAIKA NA MAWASILIANO YA SIMU KUTOKA TTCL

Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL) kuwapatia wananchi waishio vijijini zaidi ya Laki Moja mawasiliano ya Simu ifikapo mwaka 2016. Jumla USD 3.3 (sawa na Bilioni 6.8 Tsh) zitatumika kwa ajili ya kupeleka mawasiliano kwenye kata 41 zenye vijiji 41 kupitia ruzuku kutoka kwa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF) ikiwa ni awamu ya 2B.

Kata hizo ni pamoja; Oljoro –Arusha, Olmotonyi- Arusha, Olorieni – Arusha, Chikola- Dodoma, Mpalanga- Dodoma, Farkwa-Dodoma, Iduo-Dodoma, Masagalu-Tanga, Mazinde- Tanga , Mpale-Tanga, Misalai-Tanga, Ivaeny- Tanga, Kashisha-Tanga, Kashisha-Tanga, Arri-Manyara, Ayasanda-Manyara, Sigino-Manyara, Lengatei-Manyara, Bashay- Manyara, Buhendangabo- Kagera, Nyakato-Kagera, Ihembe- Kagera, Mwandu- Mwanza, Kiloleli- Simiyu, Itinje-Simiyu, Isanzu-Tabora, Neruma- Mara, Rigicha- Mara, Bwanga-Geita, Kasenga-Geita, Lumuli-Iringa, Kihesa-Iringa, Namichiga- Lindi, Galula-Mbeya, Luwalaje- Mbeya, Mbangala-Mbeya,Namkukwe- Mbeya, Kajunjumele- Mbeya, Kapele- Mbeya Mdandu-Njombe, Liparamba-Ruvuma.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa akizungumza na wadau wa makampuni ya simu pamoja na wananchi waliohudhuria uwekaji wa saini wa kupeleka mawasiliano vijijini.
Katibu Mkuu wa Wizara wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Patrick Makungu akitoa hotuba katika hafla ya uwekaji wa mikataba ya kupeleka mawasiliano ya simu vijijini
Mwakilishi wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Aumsuri Moshi akihotubia katika hafla hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF Eng. Peter Ulanga akitoa hotuba kwenye hafla uwekaji wa saini mikataba ya kupeleka mawasiliano ya simu kwenye maeneo ya vijijini.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr. Kamugisha Kazaura akitoa neno la shukhurani kwa niaba ya Makampuni ya Simu, baada ya makampuni hayo kushinda zabuni ya kupeleka mawasiliano kwenye jumla ya kata 117.

Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kamugisha Kazaura (Kushoto), Mwakilishi wa Vodacom Rosalynn Mworia (Katikati) na Mwakilishi wa Tigo Sylivia Balwire(Kulia) wakiwa katika hafla ya kusaini mikataba kwa ajili ya kupeleka mawasiliano vijijini.
Afisa Mkuu Mtendaji wa TTCL Dr Kamugisha Kazaura pamoja na wawakilishi wa makampuni ya simu ya Vodacom na Tigo wakisaini mikataba huku Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa akishuhudia tukio hilo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF Eng, Peter Ulanga akimkabidhi Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dr. Kamugisha Kazaura mkataba kwa ajili ya kupeleka mawasiliano ya simu katika kata 41.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa akiteta jambo na na Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kamugisha Kazaura.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa (Katikati), Mwakilishi wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF) Aumsuri Moshi(Kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF Eng Peter Ulanga(Kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kamugisha Kazaura (Kushoto), Mwakilishi wa Vodacom Rosalynn Mworia (Katikati) na Mwakilishi wa Tigo Sylivia Balwire.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dr. Kamugisha Kazaura kwenye baada ya kumalizika kwa uwekaji wa saini mikataba ya kupeleka mawasiliano Vijijini.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TTCL waliohudhuria hafla hiyo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad