HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 23, 2015

RANDO-KAWE JIJINI DAR YAPOTEZA MAWASILIANO YA BAADA YA MVUA

Daraja la Rando lililopo Kawe jijini Dar lionekanavyo baada ya kukumbwa na mafuriko kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha maeneo mbalimbali hapa nchini na  kupelekea usumbufu wa kutokufikika kwa baadhi maeneo ya ng'ambo ya daraja hilo, tunafahamu kwamba magari mara nyingi ndio yanasubiana kupishana lakini hapa imekuwa ni tofauti, kwani hapa Pikipiki (Bodaboda) ndio zinapishana kwa mtindo huo kwa kupita moja baada ya nyingine.
  Hali ni tete katika daraja hilo ambalo lilitengenezwa kwa msaada mkubwa wa Mbunge wa Jimbo la Kawe, Mh. Halima Mdee, lakini sasa limepoteza mawasiliano ya barabara kati ya shule ya Sekondari na ya msingi zilizopo eneo  la Rando jimbo la Kawe Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
 Muonekano wa Daraja la Rando ambako halijachukuliwa na Maji.
 Maji hayapotei njia na hapa  ndipo hupita lakini yameonyeshwa njia ndogo yakajiongeza kutafuta njia zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad