HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 3, 2015

Bondia Floyd Mayweather Jr hana mpinzani, cheki alivyomchapa Manny Pacquiao

 Bondia wa Kimarekani,Floyd Mayweather Jr akimrushia konde kali mpinzani wake, Manny Pacquiao wa Philipines wakati wa mpambano wao wa kihistoria na uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na watu wengi Duniani kote, uliopigwa mapema leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa MGM Grand Garden Arena, jijini Las Vegas, Marekani. Bondio Floyd Mayweather ameshinda mchezo huo kwa point 118-110, 116-112, 116-112 kutoka kwa waamuzi wa mchezo huo na kunyakuwa mkanda wa WBO huku akiifanya rekodi yake ya kutopigwa kufikia michezo 48.
Mchezo ulikuwa ni mkali sana na Mabondia wote walikuwa wakirushiana makonde kwa zamu.
haya angalieni wenyewe hasa wale wanaosema jamaa kabebwa.
Mabondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao wakifurahi pamoja mara baada ya mpambano wao wa kihistoria uliopigwa mapema leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa MGM Grand Garden Arena, jijini Las Vegas, Marekani.
Bondia Floyd Mayweather Jr akiwa na mikanda yake na tuzo aliyoshinda katika michezo mbali mbali

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad