HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 11, 2015

AJALI MBAYA YATOKEA MAFINGA MKOANI IRINGA LEO,ZAIDI YA WATU 40 WASADIKIWA KUPOTEZA MAISHA

Watu zaidi ya 40 wanasadikiwa kupoteza na maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya sana katika ajali mbaya iliyotokea mapema leo asubuhi,maeneo ya Changarawe,Mafinga Mkoani Iringa,iliyohusisha Lori la Mizigo na Basi la abiria la Kampuni ya Majinja lililokuwa likitokea Mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar es salaam.
Ajali hiyo imetokea baada ya Lori hilo la Mizigo lililokuwa likitokea Jijini Dar kuelekea Mbeya kuligonga na kuliangukia basi hilo wakati lililokuwa likikwepa shimo kubwa lililopo katikati ya barabara wakati wakiwa kwenye mwendo walipokuwa wakipishana. 

Hali ya Uokoaji wa maiti na majeruhi walionasa kwenye ajali hiyo bado ni tete na hasa kutokana na ukosefu wa Gesi ya kukata basi hilo kukosekana eneo lote la Mafinga,Juhudi zinafanyika ili kuweza kuokoa majeruhi pamoja na maiti.

Tunaendelea kufuatilia kwa ukaribu tukio hili ambalo ni la kusikitisha sana na ni msiba mkubwa kwa taifa,na tutaendelea kujuzana kupitia hapa hapa.
Mungu azipokee na kuzilaza mahala pema peponi roho za marehemu wote katika ajali hii na awajaalie kupona kwa haraka majeruhi wote.

Amin.

2 comments:

  1. Ni jambo lakusikitisha sana jinsi ndugu zetu walivyopoteza maisha..inawezekana ilo shimo sio limetokea from no point na kwasababu watanzania tumekuwa na tabia ya kuchukua atua baada ya tukio basi akuna jinsi

    ReplyDelete
  2. Tunaumia sana hatuna njia wakati wa shida ni lazima tusafiri yote haya tunayaweka mikononi mwako Bwana Amen

    ReplyDelete

Post Bottom Ad