Tamasha la Filamu la Nchi za Jahazi (ZIFF) limekuwa tamasha
la kwanza Afrika kukubali filamu zitumwe kupitia mtandao.
Filamu hizo zitakazoshindanishwa, sasa zitalipiwa fedha kidogo
wakati zikitumwa.
Kwa sababu ya kukua kwa mtandao wa dunia, matamasha
mengi sasa yanapokea filamu mtandaoni ili kuweza kuanza
kuzitazama filamu hata kabla muda wa kutuma filamu
haujaisha, kama ilivyokua zamani. Kwa njia hiyo wachaguaji
filamu wanapata muda mrefu zaidi wa kuzitazama filamu kwa
kituo.
ZIFF sasa haitaikubali filamu toka nchi za nje kama
haikutumwa kupitia mtandao. Hata hivyo Watanzania
watapewa upendeleo na kuruhusiwa kutuma filamu zao kama
zamani na pia hawana haja ya kulipa karo ya Euro 5 ambazo
wengine watalipia.
“ZIFF imesaini mkataba na FESTHOME, shirika lenye jukwaa
la kimataifa la upokeaji wa filamu kwa mashindano”, alisema
Daniel Nyalusi, Meneja wa Tamasha la ZIFF na kuongeza,
“ Kusema kweli hii inawapunguzia watengeneza filamu
hata gharama za utumaji filamu. Kwa kuzituma mtandaoni
tutahakikisha kazi inafanyika haraka na kuwajulisha wateja
mapema kuhusu filamu zao”.
Watu wataweza kutuma mafaili ya Vimeo yenye hadhi ya MP4
au mfumo wowote mwingine.
ZIFF ni jukwaa muhimu linalowezesha wadau wa filamu
kuonyesha filamu zao na zikapimwa kimataifa. Tamasha la
ZIFF bado linadhaminiwa na Kampuni ya ZUKU na litafanyika
Zanzibar kuanzia tarehe 18 hadi 26 Julai 2015. Mwisho wa
kupokea filamu ni Tarehe 31 Januari, 2015 hii ni pamoja na
Bongo Movie.
No comments:
Post a Comment