HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 20, 2014

#DerevaMakini: Wajibu wa taasisi, makampuni katika kupunguza ajali za mabasi ya abiria (1)

Nawasalimu nyote kwa jina la uzalendo na utaifa uliotukuka, leo katika mwendelezo wa kampeni ya #DerevaMakini ambayo inalenga kuishirikisha jamii katika kukabiliana na ajali ambazo zimekuwa mwiba kwa taifa, nitaangazia wajibu wa taasisi, makampuni na watu binafsi katika kupunguza ajali hizo.

Katika makala ya awali nilitaja orodha ndefu ya wadau wanaohusika moja kwa moja kwenye sekta ya usafiri ambao wakitekeleza sawasawa majukumu yao ajali zinaweza kupungua kama sio kukoma kabisa. Hivyo leo nitaanza na makampuni ya simu za mkononi.

Mchango wa makampuni ya simu za mkononi katika maendeleo ya sekta ya mawasiliano na uchumi kwa taifa ni mkubwa sana, lakini pamoja na manufaa hayo bado kuna madhara makubwa yanayotokana na matumizi mabaya ya simu za mkononi kwa madereva wakati wakiendesha magari yao.

Kwa mujibu wa Mtandao wa DailyMaily, takwimu zinaonyesha kuwa Dereva mmoja (1) kati ya wanne (4) wanaotumia simu zao za mkononi huku wakiendesha magari yao hupata ajali zenye ukubwa na madhara mbalimbali.

Hapa ndio swali langu linapoibuka; Je, Makampuni ya simu zamikononi yamejiwekea mikakati gani kuelimisha wateja wake juu ya madhara ya matumizi ya simu wakati wakiendesha? Au wanachojali wao ni kutengeneza faida tu pasipo kuangalia madhara yanayowakumba wateja wao?

Tumeona ushiriki wa baadhi ya makampuni hayo katika wiki za nenda kwa usalama yakihimiza usalama barabarani, lakini ingefaa zaidi kama ushiriki wao ungekuwa endelevu, pengine wangeweka hata jumbe kwenye kadi za muda wa maongezi ili kila anayenunua muda huo aweza kupata elimu Fulani.

Sote ni mashahidi kwa makampuni yanayouza vileo, sheria inayalazimisha kuweka onyo juu yamadhara yanayoweza kumpata mtumiaji endapo atatumia bidhaa hizo vibaya, jambo ambalo  linawezwa kuigwa na makampuni ya simu nayo yakaanza kutoa onyo la matumizi mabaya ya simu kwa madereva wanapoendesha.

Ni mtazamo tu, na wewe msomaji kupitia forum hii unaweza kutupia mawazo, mtazamo, ushauri na hata maswali yako ukizingatia mada aliyetajwa hapo juu, maoni yako tutayatumia kwenye mada ifuatayo.

Wiki ijayo tutaendelea kuwaangalia wadau wengine na majukumu yao wakiwemo Askari wa Usalama Barabarani, Madereva, Abiria, Wamiliki wa vyombo vya usafiri, Sumatra, Vyombo vya habari, Tanroads, Miundombinu , TBS, Wauzaji wa magari, Sheli za mafuta na vipuli vya magari. 

Kampeni hii ya #DerevaMakini inayolenga kupunguza ajali za barabarani ikijikita zaidi kwenye mabasi ya abiria imewezeshwa na Michuzi Blog, Tabianchi Blog na Transevents Marketing

Kwa taarifa zaidi tembelea Dereva Makini

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad