HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 29, 2014

MH. PINDI CHANA ATEMBELEA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI ARNAUTOGLU, DAR

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb.), leo tarehe 28 Oktoba, 2014 amefanya ziara katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu – Ilala, Dar es salaam, kwa lengo la kukagua maendeleo ya utoaji wa mafunzo kwa wananchi. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu hutoa mafunzo ya muda mrefu, muda mfupi na mafunzo nje ya chuo, ambayo yote yamelenga katika kutoa stadi na maarifa mbalimbali yanayowawezesha washiriki kupata ujuzi ili waweze kujiajiri wenyewe au kuajiriwa katika Taasisi mbalimbali kwa lengo la kuzalisha mali na hivyo kujiongezea kipato na kupunguza umaskini. Kwa upande wa mafunzo ya muda mrefu asilimia kubwa ya Wanafunzi wanaojiunga na Chuo hiki ni watu wenye ulemavu, wengi wao wakiwa na ulemavu wa akili.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi na uongozi wa wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu, Ilala – Dar es salaam , wakati alipofanya ziara Chuoni hapo leo Oktoba 28, 2014.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana(Mb.) akiongea na watumishi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu ( hawapo pichani), wakati alipofanya ziara Chuoni hapo, leo Oktoba 28, 2014. Kushoto ni Bwana Stephen Saro, Afisa Elimu Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na Kulia ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu, Bibi Pulcheria Ndamugoba.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana(Mb.) akikagua mazingira ya utoaji wa mafunzo katika madarasa ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu, ikiwa ni pamoja na kuhojiana na washiriki wa mafunzo (hawapo pichani), wakati alipofanya ziara katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu - Ilala, Dar es salaam, leo Oktoba 28, 2014. Kulia ni Bwana Stephen Saro, Afisa Elimu Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu, Bibi Pulcheria Ndamugoba.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb.) akiangalia mafunzo kwa vitendo yaliyokuwa yakitolewa kwa washiriki wa darasa la Uashi, katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu - Ilala, Dar es salaam, leo Oktoba 28, 2014.
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu, Bibi Pulcheria Ndamugoba akitoa ufafanuzi kuhusu eneo la chuo kwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb.) wakati alipofanya ziara katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu - Ilala, Dar es salaam, leo Oktoba 28, 2014.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad