HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 1, 2014

KUMBUKUMBU

Marehemu Mzee Joseph Mturi Mahemba
(1955-2012)

Mpendwa Baba yetu, Joseph Mturi Mahemba Hatimaye siku, Miezi imepita hadi hii leo ambapo imetimia Miaka miwili (2) tangu ulipotutoka ghafla usiku ule wa siku ya jumatano ya tarehe moja ya Mwezi Agosti, 2012 na kutuachia huzuni kubwa.

Japokuwa haupo nasi hapa duniani lakini tupo nawe kiroho kwa kuendeleza mema yote uliyotufundisha na kutuasa.

Tunakukumbuka kwa Upole, Upendo, Busara na Ukarimu uliokuwa nao kwa familia na Marafiki. Mwongozo na matendo yako yataendelea kuwa dira kwetu Daima unakumbukwa sana na Mkeo Rose Joseph, dada zako Theresia, Karaghita, Wankuru na Mnaga, wanao wapendwa Michael, Mkami, Niwa, Sagana, Mary, Geofrey, Nyakaho, Lecardia na Pricilla, na wajukuu zako wote.

Ibada Maalum ya Maombi itafanyika tarehe 03/08/2014 Saa 2.00 asubuhi kwenye kanisa katoliki la Mt Maurus Kurasini, Dar es Salaam.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake libalikiwe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad