HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 28, 2012

Maelfu ya Watanzania wamzika Marehemu Sharo Milionea jijini Tanga leo

Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea enzi za uhai wake.
Waumini wa Kiislam wakiwa katika Ibada ya Kuuswalia Mwili wa Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea aliefariki kwa ajali ya Gari hivi karibuni huko Muheza,Mkoani Tanga.
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea likiwasili Nyumbani tayari kwa Taratibu za Mazishi yaliyofanyika leo kwenye Kijiji cha Lusanga,Wilayani Muheza,Mkoani Tanga.
udogo ukitupiwa kaburini wakati wa mazishi ya Msanii wa Muziki na Filamu hapa nchini,Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea,ambayo yalihudhuliwa na Watu mbali mbali hapa nchini,wakiwemo viongozi katika kijiji cha Lusanga,Muheza Mkoani Tanga.
Muigizaji Maarufu hapa nchini,Mzee Athuman Amri a.k.a King Majuto ambaye ni Baba Mdogo wa Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea akitupa mchanga kaburini wakati wa Mazishi ya Sharo yaliyofanyika leo katika kijiji cha Lusanga,Muheza Mkoani Tanga.
Vijana wakiwa wamepanda mnazi kuona mazishi ya Msanii wa Muziki hapa nchini,Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea katika kijiji cha Lusanga,Muheza Mkoani Tanga.
Waombolezaji wakimsaidia mwenzao aliyepoteza fahamu msibani.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akitoa pole za Chama mara baada ya kumalizika kwa mazishi ya Msanii wa Muziki na Filamu,Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea katika kijiji cha Lusanga,Muheza Mkoani Tanga.
Kiongozi wa Tanzania Fleva Unit,Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA akitoa salam kwa niaba ya Wanamuziki wa Bongofleva.
Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subra Mgalu akisoma salam za EOTF.
Baadhi ya wasanii msibani, Lusanga.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania,Jackson Mbando (katikati) akiwa pamoaja na baadhi ya wasanii wa Muziki wa BongoFleva wakati wa Mazishi ya Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Milionea katika kijiji cha Lusanga,Muheza Mkoani Tanga.Picha na Bashir Nkoromo.

34 comments:

  1. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe

    ReplyDelete
  2. Angepewa nafasi ya mwisho aseme neno angesema "msinirushie udongo meeen"
    RIP

    ReplyDelete
  3. Innallillah wainna ilaayhy raajiuun

    ReplyDelete
  4. Mwanga wa milele umpe e bwana , apumzike kwa amani.

    ReplyDelete
  5. mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni....Amen

    ReplyDelete
  6. Inna Lillah Waina Illaih Rajoon

    Tunakuomba Allah S.W umpumzishe mahali pema patulivu peponi.

    ReplyDelete
  7. Pumzika kwa Amani Kaka wote tupo njia moja.

    ReplyDelete
  8. Inna lillahi wa inna ilayhi rajium..Mungu atupe subra watanzania wote....kumbukeni swala na ibada..dunia ni njia tu...kilichobakia ni kumuombea dua sharo..ndio zitamfikia...na tushukuru mungu..nawaombea family yake subra...na wamuombee...hii njia sote tutapita jamani..lakini...uchungu..inaniuma.....Allah Kareem

    ReplyDelete
  9. Msibani na sare za CCM si ukenge huo?

    ReplyDelete
  10. ALIKUWA ANATANGAZA AIRTEL MONEY KWA NINI HAKUPELEKA PESA KWA NJIA HIYO??
    NI JUHUDI BILA MAARIFA KAMA WALIVYO WENGI TANZANIA

    ReplyDelete
  11. Ninaamini ameenda kuanza maisha mengine ya ulimwengu mwingine.namtakia kila lenye kheri,tutamkumbuka daima.lala salama Hussein.

    ReplyDelete
  12. Tuendelee kumwombea Sharo, Bwana ampumzishe kwa amani, Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake libarikiwe. Amen

    ReplyDelete
  13. NAJUA HAMTA-PIBLISH LAKINI NDIO HALI HALISI
    SHULE HAKUNA TANZANIA!

    ReplyDelete
  14. Innalillah wainaillaih rajiuun, Mungu amlaze mahali pema peponi, AMEEN

    ReplyDelete
  15. inallillah waina illah rajoon.

    Kila nafsi itaonja mauti, mwenyezi mungu amlaze mahala pema peponi, amina, ampe subra mamake.

    ReplyDelete
  16. INNA LILLAHI WAINNA ILLAHI RAJIUN. MWENYE EZIMGU AIWEKE ROHO YAKE PAHALA PEMA INSHALLAH. AMSAMEHE MADHAMBI YAKE YOTE. AMEEN

    ReplyDelete
  17. WALIOVAA SARE ZA CCM WANALAO JAMBO LABDA WALIKUWA KWENYE KAMBENI WAKASAHAU KUWA NI MSIBA

    ReplyDelete
  18. Ndugu uliyesema 'si angetumia AIRTEL' sijui unaishi Dunia gani?!! Yaani na mzazi wake angemuona kwa AIRTEL? Siyo kila jambo ni utani bwana behave.

    ReplyDelete
  19. wote tupo njia hii,mwanadamu siku za maisha yake ni kama MAUA huchanuwa na kusinyaa,tujiombee na sisi kwani hatujui siku wala saa tuwe tayari.

    ReplyDelete
  20. Tujiandae wote nisafari yetu, cha msingi ni kujiandaa vizuri na Mungu, tusiache kufanya Ibada na kumshukuru Mungu kwa Neema aliyotujalia kuwa hai.

    ReplyDelete
  21. Acha upimbi wew hata kama airtell money asimchek bi mkubwa ndio ulivyo ambia au unafiki

    ReplyDelete
  22. God bless you my brother rest in peace Inshallah... Mwenyezi mungu Akusameheme mabaya yote..

    ReplyDelete
  23. hakuna msiba usiokuwa na wenyewe...hao waliofika msibani na jezi za vyama au chama hawatofanikiwa lengo lao pia nape si kiongozi wa serkali ni wa ccm,kachemka kuja kueneza sera za siasa za ccm ktk mazishi ya waislam...na rangi ya kijan ktk shuka la jeneza haiwakilishi u-ccm bali kijani ndo rangi iwakilishayo uislam.mmebugi nape,na inshaalah mwenyezi mungu atazidi ku2fumbua macho watz,R.I.P HUSEIN BIN RAMADHAN BIN MKIETY

    ReplyDelete
  24. Tuko safarini, tuombeane kila iitwayo leo hatujui siku wala saa. Raha ya Milele umpee ee Bwana....

    ReplyDelete
  25. Aya bana,,tumewasikia wote mliotoa maoni,,(mumetumia haki yenu ya kikatiba),,sina la zaidi (Ila dogo apumzike kwa amani)

    ReplyDelete
  26. inackitisha hasa huyo alosema atumie airtel money nai mpuuzi asie na ubinadam na hana akili hata kidogo na ningekua na uwezo aiseeee angejuta RIP SHARO WE WILL ALWAYS LOVE YOU

    ReplyDelete
  27. M/MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PAHALI PEMA PEPONI AMIN KWA SOTE,M/MUNGU UWAONDOSHEE MAJONZI FAMILIA YAKE

    ReplyDelete
  28. rest in peace sharo,, we will mic u

    ReplyDelete

Post Bottom Ad