MKCT Love
Thursday, March 05, 2015

Tabora wafurahia huduma za madaktari Bingwa

Na Grace Michael, Tabora

WAGONJWA waliofika na kupata huduma za Madaktari Bingwa ambao wapo kwenye mpango unaoendeshwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wamefurahia huduma hizo na kusema kwamba zimeokoa fedha nyingi ambazo wangetakiwa kuzitumia kusafiri kufuata huduma hizo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika Hospitali ya Mkoa wa Tabora, Kitete, walisema kwamba ujio wa Madaktari hao umewasaidia kupata huduma nzuri na zinazohitajika bila ya usumbufu wa aina yoyote na wala kutumia gharama kubwa.

“Kwa upande wangu nashukuru mno kwani nilifika hapa nikiwa na hali mbaya sana, nilikuwa siwezi hata kula wala kutembea, lakini nipofika na kuonwa na daktari Bingwa na kunipa huduma nina nafuu kubwa mno kwani naweza kula na kuzungumza vizuri,” alisema Bw. Shukuru Jumanne (33) Mkazi wa Ipuli mkoani Tabora.

Mgonjwa huyo alipata huduma ya kutolewa maji kwenye kuta za moyo ambayo yalikuwa yakimsabishia maumivu makali na kushindwa kupumua vizuri. Mgonjwa mwingine ambaye naye alipata huduma hiyo, Bi. Halima Juma (49) mkazi wa Ipuli, Tabora alisema kuwa ana faraja kubwa baada ya kupata huduma ya kutolewa maji ambapo sasa anaweza kupumua vizuri ikilinganishwa na mwanzo.

“Sikuwa na uwezo wa kufuata huduma hizi mbali hivyo ujio wa hawa wataalam kwangu ni kama muujiza, namshukuru sana Mungu kwa kuwaonesha NHIF mpango kama huu,” alisema Bi. Halima.

Mbali na wagonjwa hawa, pia ndugu wa wagonjwa ambao walikuwa na ndugu zao wakiwa kwenye chumba cha upasuaji, waliupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kuona umuhimu wa kuleta wataalam hao mkoani Tabora. Walisema kuwa huduma kama za upasuaji na huduma zingine ambazo walitakiwa kuzifuata Muhimbili au Bugando wamezipata hospitalini hapa bila ya usumbufu wowote.

Wamesema kuwa kitendo cha madaktari bingwa kuja mkoani hapo kimewapunguzia gharama ambazo wangetakiwa kuzitumia, hivyo wameuomba Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuendelea na utaratibu huo ili kukomboa maisha ya Watanzania wengi wanaoishi katika mikoa ya pembezoni.

Mpaka sasa jumla ya wagonjwa…..wameonwa na Madaktari Bingwa huku wagonjwa ……wamefanyiwa upasuaji tangu zoezi hili lilipoanza siku ya Jumatatu.
Wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakihakikiwa nyaraka zao kabla ya kuingia kupata huduma za Madaktari Bingwa.
Wahitaji wa huduma za kitaalam wakisubiri kuwaona madaktari bingwa.
Baadhi ya ndugu wa wagonjwa na wagonjwa wakisubiri kumuona daktari Bingwa wa Masuala ya Moyo.
Dk. Peter Kisenge kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili akimjulia hali mgonjwa Shukuru Jumanne ambaye alimpa huduma ya kumtoa maji kwenye kuta za moyo.
Madaktari wakijiandaa kumhudumia Mgonjwa Halima Juma ambaye alikuwa na maji kwenye ukuta moyo.
Wananchi wakiwa na subira ya kukutana na wataalam.

Mh. Lowasaa akutana kwa mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nchi za Nje,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Mh. Dianna Melrose aliyefika ofisini kwake leo kwa mazungumzo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nchi za Nje,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Mh. Dianna Melrose ofisini kwake,jijini Dar es salaam leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nchi za Nje,Mh. Edward Lowassa akiagana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Mh. Dianna Melrose mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

KIJIJI CHA GONGONI WILAYANI KILOSA WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, WANAWAKE WAPATA HATI MILIKI ZA ARDHI

Angelina Mziray Katibu Mkuu wa Women and Poverty alleviation in Tanzania  , Akiwakaribisha wageni Mbalimbali waliofika katika Sherehe za Kuazimisha Siku ya Wanawake Duniani ambapo wao wameadhimisha mapema,Katika Ufunguzi Alisema kuwa Shirika lisilo ka Kiserikali la Waupata wakishirikiana na OXFAM wamesaidia Kijiji hicho katika kuleta maendeleo mbalimbali Tangu mwaka 2006 ikiwa ni pamoja na Kilimo cha mpunga, Matumizi Bora ya Ardhi, Ambapo Pia aliwashukuru OXFAM kwa kuleta ufugaji bora wa kuku wa kienyeji, na ujenzi wa masoko mawili ya kisasa, Pia kusaidia wanawake kupata hati milili za Ardhi ambapo wanawake 186 watapata Hati hizo. Mwisho alishukuru taasisi zengine zisizo za Kiserikali ikiwemo Mviwata,Ungo,Tupawaki pamoja na Mwayodeo kwa jitihada zao za kusaidia wanawake na wanakijiji cha Gongoni katika maendeleo ya kijiji hicho.
 Mmoja wa Mashuhuda Juliana Bi. Salum ambaye amepata haki Miliki ya Ardhi akielezea Jinsi gani ambavyo itamsaidia katika Maendeleo yake na jamii kwa ujumla.
Mshereheshaji MC Chadieli G. Senzighe akiendelea kutoa Mwongozo katika Sherehe hizo.
 Elizabeth Luoga ambaye pia amepata Hati Miliki ya Ardhi akielezea Furaha yake na Ushuhuda wake kwa kuwashukuru OXFAM kwa jitihada kubwa walizo zifanya na wanazo zifanya ili wanawake wapate umiliki wa Ardhi amewashauri wanawake kuwa umiliki wa Ardhi unawezekana.
 Kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Gongoni, Kilichopo Kata ya Rudewa Tarafa ya Kimamba Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro Bi. Grace Robertson Kanwakaita akitoa utambulisho kwa wageni mbalimbali ambao walifika katika Sherehe ya wanawake wakiwemo, Wakulima na wamama wafugaji walio katika eneo hilo,Opata,shirikisho la Ardhi,OXFAM, Mviwata,Ungo na wagani wengine waalikwa.

NENO LA LEO MTAANI


Wednesday, March 04, 2015

UFAFANUZI JUU YA HALI YA AFYA YA NAIBU SPIKA

Naibu Spika wa Bunge,Mh. Job Ndugai.

Mvuvi katika kisiwa cha Yozu wilaya ya Sengerema Aibuka na Toyota IST ya Airtel

Kaimu Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa wa Airtel Bwana David Wankuru akimkabithi gari aina ya Toyota IST bwana Kijiji Gweso ambaye ni Mvuvi na mkazi wa wilaya ya Sengerema Mwanza mara baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi akishuhudia ni Afisa Uhusiano wa Airtel,Bi. Jane Matinde.
Mshindi wa gari kupitia promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Bwana Kijiji Gweso akifungua gari mara baada ya kukabidhiwa gari na Airtel mara baada ya kuibuka mshindi, Bwana Gweso ni Mvuvi na mkazi wa wilaya ya Sengerema Mwanza. akishuhudia ni Kaimu Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa wa Airtel David Wankuru.
Mshindi wa gari kupitia promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Bwana Kijiji Gweso akiwa ndani ya gari yake mara baada ya kukabidhiwa gari na Airtel mara baada ya kuibuka mshindi, Bwana Gweso ni Mvuvi na mkazi wa wilaya ya Sengerema Mwanza.
Kaimu Katibu wa Wilaya ya Sengerema Bwana Aaron L Laizer ( wa pili kushoto) akimkabithi gari aina ya Toyota IST bwana Kijiji Gweso ambaye ni Mvuvi na mkazi wa wilaya ya Sengerema Mwanza mara baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi akishuhudia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde na Kaimu Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa wa Airtel Bwana David Wankuru.

Mkazi wa wilaya ya sengerma na mvuvi katika kisiwa cha Yozu bwana Kijiji Gweso Jana amekabithiwa gari aina ya Toyota IST na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel mara baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya Airtel yatosha zaidi.

Akiongea wakati wa halfa ya kukabithiwa gari lake Bwana kijiji Gweso alisema” nilipopigiwa simu na Airtel nilipuuzia sikuamini kabisa kama nimeshinda gari mpaka ndugu zangu waliponipigia na kunihakikishia kuwa mimi nimetangazwa mshindi ndipo nilipoenda ofisi za Airtel na kukuta kweli nimejishindia. Mimi ni mvuvi na mke na watoto wawili na nilinunua kifurushi cha Airtel yatosha cha mia tano tu na furahi sana kushinda gari hili kupitia promosheni hii”.

STAILI MPYA YA KUPISHANISHA MAGARI


WAZEE WA KAZI WAKIWAJIBIKA

Kama ulikuwa hujui,basi siku hizi wabeba mizigo wanapigilia kama madaktari vile.

VUVUZELA ORIJINALI


alaaa kumbe hiki kikapu ndio kazi yakeee....???

Siku zote nilikuwa nikijiuliza kuwa hivi vikapu kwenye pikipiki vina kazi gani??,leo ndio nimepata jibu lake sasa.

WAKITOKA SOKONI


HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA YAZIDUA UPIMAJI USIKIVU WA WATOTO WACHANGA

Waziri wa Afya wa Zanzibar Rashid Seif Suleiman akikata utepe kuzindua mpango wa upimaji usikivu wa watoto wachanga katika hafla iliyofanyika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar, wa kwanza (kushoto) mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Ghirmay Andemichael na (wakatikati) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Halima Maulid Salum.
Daktari Asma Ame Hassan akimpima usikivu mtoto Nour Sabri Al hilal katika uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto wachanga hafla iliyofanyika Hospitali kuu ya Mnazimmoja.
Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman akisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto wachanga. (kulia) Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Dkt. Jamala Adam Taib na (kushoto) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Halima Maulid Salum.
Mjumbe wa Bodi ya ZOP Yahya Mohammed Slim akitoa maelezo kuhusu Jumuiya hiyo inavyotoa huduma za kijamii vijijini katika usinduzi wa kuwapima usikivu watoto wachanga.
Wafanyakazi wa Afya waliopatiwa mafunzo maalum ya kuwapima usikivu watoto wachanga wakimsikiliza Waziri wa Afya (hayupo pichani) katika uzinduzi huo.
baadhi ya wageni walioalikwa katika uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto wachanga wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika Hospitali ya Mnazimmoja. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

MAANDALIZI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA MAAFISA NA ASKARI WA JESHI LA MAGEREZA YAPAMBA MOTO

Sehemu ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa katika mazoezi makali katika mitaa ya mji wa Moshi ikiwa ni maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro ifikapo Machi 6,2015. Katikati (mwenye vazi jeupe) ni Kamishna Msaidizi wa Magereza Alexander Mmasy kutoka Makao Makuu ya Magereza, wa kwanza kulia ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza Mbezi Ramadhani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga na wa kwanza kushoto ni Mkaguzi wa Magereza Jamhuri Yassin kutoka Makao Makuu ya Magereza, Dar es salaam.
Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa katika mazoezi ya kutembea katika viunga vya Manispaa ya Moshi ikiwa ni maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro mnamo Machi 6, 2015. Kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Magereza Vicent Magessa kutoka Gereza Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Mkaguzi wa Magereza Tumaini Kihampa na Mkaguzi wa Magereza Jamhuri Yassin wote kutoka Makao Makuu ya Magereza.
Maafisa na Askari na baadhi wa watumishi raia wa Jeshi la Magereza wakiwa katika mazoezi makali ya kupita katika njia ngumu ikiwa ni maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro ifikapo Machi 6, 2015. Wa sita kutoka mbele ni Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Magereza Estomiah Hamis na wa mwisho ni Mkaguzi wa Magereza Abas Mikidadi.
Maafisa na Askari na baadhi wa watumishi raia wa Jeshi la Magereza wakiwa katika mazoezi makali ya kupita katika njia ngumu ikiwa ni maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro ifikapo Machi 6, 2015.
Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa katika mazoezi ya viungo baada ya kutembea na kukimbia katika viunga vya Manispaa ya Moshi ikiwa ni maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro mnamo Machi 6, 2015.
Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakipata kifungua kinywa baada ya mazoezi mazito ya maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro ifikapo Machi 6,2015. Maafisa hao wako kambini eneo la Gereza Karanga mjini Moshi.
Baadhi wa washiriki wa Kilimanjaro Marathon Machi 1, 2015 mbio ambazo baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza walishiriki ikiwa ni maandalizi ya kupanda Mlima Kilimanjaro mnao Machi 6, 2015. Picha zote na Mkaguzi wa Magereza Deodatus Kazinja

TAARIFA YA DAWASCO JUU YA HITILAFU KATIKA MTAMBO WA MAJI WA RUVU JUU

Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linawatangazia  wakazi wa KIMARA na TABATA; Miji ya Kibaha na Mlandizi mkoani Pwani  kuwa, tangu Jumapili ya Tarehe 01/03/2015 Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Juu  umepata hitilafu baada ya bomba la Majighafi (Raw-Water) kuachia kwenye moja ya chemba ya kuchukulia Maji eneo la Mtamboni.
  
Hali hii imelazimu kuzima Mtambo wa Ruvu Juu. 

Mafundi wa DAWASCO wanaendelea na matengenezo ili kuhakikisha  Huduma ya  Maji inarejea katika hali ya kawaida ifikapo  siku ya Ijumaa 06/03/2015.

Wakazi wa maeneo yafuatayo wameathirika na hitilafu hii; MLANDIZI, KIBAHA, KIBAMBA, MBEZI, KIMARA, UBUNGO, CHUOKIKUU, KIBANGU, RIVERSIDE, BARABARA YA MANDELA, TABATA, NA SEGEREA.

KWA TAARIFA ZAIDI PIGA SIMU KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA NAMBA 022 5500 240-4 au 0658-198889
DAWASCO INAWAOMBA RADHI KWA USUMBUFU AMBAO NI WA DHARULA.

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU
“DAWASCO TUTAKUFIKIA”

KATIBU MKUU KIONGOZI AFURAHISHWA NA UWEPO WA SACCOS MAKAZINI

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipokea kitabu chake cha uanachama toka kwa Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio (wa tatu toka kulia). Wengine ni Katibu wa wa ushirika huo Bw. Benedicto Damiano (wa pili kulia), Mtunza Hazina Bi. Judith Medson ( wapili kushoto) na Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga kulia,wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akionesha kitabu chake cha uanachama baadas ya kukabidhiwa na Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio wakishuhudiwa na Katibu wa wa ushirika huo Bw. Benedicto Damiano, Mtunza Hazina Bi. Judith Medson ( wapili kushoto) Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga kulia,wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipata maelezo ya matumizi ya kitabu cha uanachama toka kwa Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga kulia, wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam. Kati ni Makamu Mwenyekiti wa ushirika huo Bw. Deodatus Gudio.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) akimsikiliza Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga (wa pili kulia) akimuelezea mikakati ya ushirika huo wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam. Wa pili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio, akifuatiwa na Katibu wake Bw. Benedicto Damiano na kulia ni Mtunza Hazina Bi. Judith Medson.PICHA NA IKULU

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amefurahishwa na uwepo wa vyama vya Ushirika vya Akiba na mikopo (SACCOS) katika taasisi na idara za serikali, akisema kuwa hilo ni jambo la maana kwa kuwa inatoa fursa kwa watumishi kuwa na kipato cha ziada kitachosaidia kuwaletea ahueni kwani mishahara pekee haikidhi matakwa yao yote.

Amesema SACCOS ni ​kama ​ benki ya mtu mnyonge, na kusisitiza kwamba mifuko ya aina hiyo inaposimamiwa vizuri faida yake kwa wanachama ni kubwa sana kwani humpa mtumishi ahueni na kumfanya afanye kazi kwa moyo na bila wasiwasi ama usongo wa mawazo.

Watu 35 wanadaiwa kupoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha huko Kahama,Shinyanga

Zaidi ya Watu 35 wanadaiwa kupoteza maisha na wengine 55 kudaiwa kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na nyumba zao kufuatia mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha usiku wa kuamkia leo, katika kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Tunaendelea kufuatilia tukio hilo kwa ukaribu na tutapeana habari kamili hapo baadae kidogo.

CHANZO: RADIO ONE

TASWIRA MWANANA KABISA KUTOKEA BONDE LA JANGWANI JIJINI DAR LEO

Nafasi Ya Matangazo